13 November 2013

IRENE UWOYA AENDA KWA MATUMLA KUJIFUNZA NGUMI..!! TAZAMA PICHA...!!


MSANII wa filamu wa kike Bongo Irene Uwoya yupo katika maandalizi ya kuanza mazoezi ya ngumi baada ya kumpata mwalimu ambaye ni Bondia maarufu Rashid Matumla ‘Snake Boy’ akiongea na FC Irene kasema kuwa ameamua kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiweka vema na kulinda nafasi yake ya uigizaji kwani amegundua wasanii wengi wanapoteza mvuto kwa kujiachia kwa unene.
Irene Uwoya
Irene Uwoya katika pozi
Irene Uwoya, Rashid Matumla, Francis Cheka, Lumole Matovolwa
Irene Uwoya akiwa na timu ya mabondia na Biggie
Irene Uwoya, Rashid Matumla
Irene Uwoya akiwa na Mwalimu wake Snake Boy kwa ajili ya kujifua.
“Nimejipanga kwa kufanya mazoezi ya nguvu chini ya mwalimu wangu Rashid Matumla na nipo fiti kwa ajili ya kujifua najua kuigiza ndio ajira yangu lakini nikijiachia na kunenepa bila mpango nitaanza kucheza nafasi za akina bibi muda si mrefu na najiona mwili
unavyoninyemelea sitaki manyama uzembe,”anasema Irene Uwoya.
Irene ni moja kati ya wasanii wakali wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamau Bongo huku pia akiwa ni moja kati ya watayarishaji wa filamu wanadada akiwa ameandaa filamu la Apple filamu iliyotengenezwa kwa gharama kubwa na kuwashirikisha wasanii kama Patcho Mwamba, Baba Haji na wasanii wengine wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname