HALI ya mwanamke aliyepigwa risasi na polisi katika Benki ya CRDB
mjini hapa, Violet Lyapa (30) bado ni tete huku taarifa zake zikifanywa
kuwa siri kubwa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hospitali ya Selian, Violet bado
amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) huku hali yake
ikibadilikabadilika.
Pamoja na kwamba tukio hilo limechukua siku zaidi ya tano bado hali ya Violet inafanywa kuwa siri nzito.
Mwanamke
huyo amewekewa ulinzi mkali katika wodi aliyolazwa lakini mmoja wa
wauguzi wa hospitali hiyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe,
amesema hali ya majeruhi huyo imekuwa ikibadilika kiasi cha kulazimika
kumpa uangalizi maalum.
Jeshi la polisi mkoani hapa limekuwa na kigugumizi kutoa taarifa juu
ya tukio hilo na hatua zipi zimechukuliwa juu ya uhalali wa umiliki wa
silaha iliyotumia kuwatishia polisi baada ya kukuta gari lake limetolewa
upepo.
Aidha, katika hali inayotia shaka kigogo wa ngazi za juu mkoani
Arusha amekuwa akimjulia hali mara kwa mara majeruhi huyo hasa nyakati
za usiku na taarifa zilizoenea zinasema kigogo huyo ana uhusiano wa
karibu na majeruhi huyo.
Pia, baadhi ya ndugu wa majeruhi wamelalamikia kuzuiwa kumuona ndugu yao na kutakiwa kuonesha vitambulisho
No comments:
Post a Comment