Baada
ya kupondwa na Huddah Monroe kuwa ‘amepigika’ mfalme wa bling,
Rapcellency Prezzo ameamua kujibu mashambulizi na kusema uhusiano wake
na Huddah ulikuwa wa kufanya mapenzi tu, basi.
Kwenye
interview na Heads Up, Prezzo aliweka wazi kuwa ni kweli aliwahi kuwa
na uhusiano wa muda mfupi na aliyekuwa mwakilishi huyo wa Kenya kwenye
Big Brother Africa mwaka huu.
“Tuliwahi kukutana kama mara tatu hivi nadhani alipenda alichokipata. Alinogewa,” Prezzo aliimbia Heads Up.
Anadai kuwa Huddah amechukia kwasababu hakutaka kuendelea naye.
“Huddah
ni kama mali ya serikali. Amelala na karibu dunia nzima. Unadhani rais
anaweza kutulia na mwanamke kama huyo,”alihoji Prezzo. Alidai pia kuwa
Huddah amekuwa akiwasumbua wanawake wote wengine aliowahi kuwa na
uhusiano nao.
“Sijawahi kumjibu, lakini utagundua kuwa alimshambulia Goldie na Diva wa Tanzania.”
Wakati huo huo, Huddah amekuwa akitweet majibu ya kile alichokisema Prezzo.
Credit -Bongo5.com
No comments:
Post a Comment