09 November 2013

HII NI LIST YA WASANII WA HIP HOP BONGO WENYE MAENDELEO KIMAISHA NA WALIODHIISHA KUWA HIP HOP SIO UHUNI..!!


Pamoja na kwamba imepungua kidogo, bado kasumba ya kwamba hip hop ni uhuni imeendelea kuwa na makazi kwenye akili za Watanzania wengi. Hata kwa wazazi wengi, vijana wanaofanya hip hop wameendelea kuonekana kama wahuni na wavuta bangi.
Japokuwa ni kweli kwamba maisha ya baadhi ya wana hip hop,yamekuwa yakiipa nguvu zaidi kasumba hii, wapo rappers smart ambao kwa matendo yao, maisha yao, elimu zao na mafanikio yao, akili walizonazo na namna wanavyojua kujenga hoja, wameishinda nguvu kasumba hii.
Hawa ni miongoni mwa rappers hao.

Joseph Mbilinyi aka Sugu
MR SUGU
Kutoka kwenye hip hop hadi bungeni. Sugu aliwaacha midomo wazi watu wengi baada ya mwaka 2010 kushinda kiti cha ubunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA. Wakati wa kampeni, hata wapinzani wake walikuwa wakitumia propaganda ya kumwelezea mbunge huyo kama mhuni, japo wananchi wa Mbeya hilo hawakulijali. Tangu aingie bungeni, Sugu amekuwa mmoja wa watetezi wazuri wa wananchi wa Tanzania na ni mtu mwenye hoja, na mwanasiasa mzuri.
Profesa Jay
p_profj
Unaweza kuwa umeshahau, lakini nyimbo za Profesa Jay, hususan, nyimbo tatu zilizofuatana kimaudhui (trilogy) Ndio Mzee, Kikao cha Dharura na Nang’atuka zilikuwa na ‘impact’ kubwa kisiasa nchini. Zilieleza hali halisi ya jinsi wanasiasa walivyo na ahadi tamu wakati wa kampeni ambazo hushindwa kuzitekeleza waingiapo madarakani. Unaanza vipi kuziita nyimbo hizi ni za uhuni?

AY
AY
Kutoka kuwa rapper hadi kuwa ‘business mogul’. Mwaka jana AY aliishawishi kampuni ya Airtel Afrika kumteua kuwa balozi wake, akiungana na wasanii wengine akiwemo Papa Wemba. Kama rap ingekuwa ni uhuni siamini kama, kampuni kubwa kama hiyo ingempa heshima hiyo kubwa.
Leo hii AY, akiwa CEO wa Unity Entertainment, amekuwa akifanya biashara na makampuni makubwa nchini na kukaa mezani na watu wenye maamuzi katika makampuni hayo. “Tulianza tukiwa hatuna deal kabisa ingawa tumefungua ofisi, leo hii tunahandle accounts za makampuni,” AY aliiambia Bongo5 hivi karibuni kuhusiana na mafanikio ya kampuni yake.

Fid
Mwana FA, Fid Q, AY, Arthur na mshikaji
Niliwahi kumuelezea Fareed kwenye makala yake mwenyewe (Makala: ‘Siri ya Mchezo’ ya kwanini Fid Q ni ‘Hip Hop Genius’) ambapo sehemu ya yale niliyoandika yalisema: Wakati mwingine mawazo na kile anachokiandika Fid Q, kinaweza kumfanya mtu anayechukua Phd ajihisi mwanafunzi tu mbele yake. Pengine ni kwasababu, rapper huyu wa Mwanza anapenda sana kusoma vitabu. Kutokana na ukweli kuwa, Watanzania wengi hatuna utamaduni wa usomaji vitabu kujiongezea maarifa, ni ngumu kuyafananisha mawazo yake na ya rapper mwingine yeyote Tanzania, hata aliyesoma kiasi gani.”

Nick wa Pili
niki-wa-pili-533x800
Hakupata nafasi ya kuwa mmoja wa wasemaji kwenye semina za fursa za Clouds FM bure. Elimu yake na uwezo wa kupambanua mambo kisomi ndio uliwavutia waratibu wa semina hizo na kumpa nafasi. Kwa wale waliohudhuria semina hizo, wanajua upeo mkubwa wa rapper huyu wa Weusi. Akiwa na shahada yake ya pili kibindoni, Nick wa Pili amedhamiria kufanya makubwa.
“Nafikiria kufanya projects, nafikiria kuwa na media house ya kwangu, nafikiria kuwa na NGO, na nafikiria kujiajiri kupitia muziki pia,” Nick aliiambia Bongo5 hivi karibuni.

Mwana FA
IMG_0909 (533x800)
Kutoka kuwa rapper hadi kuwa mwajiriwa benki, kuacha na kuwa mjasiriahiphop. Hamis Mwinjuma ana shahada zake mbili kibindoni za masuala ya biashara na amekuwa akionesha nia ya kutaka kuendelea na kitabu zaidi. Akiwa na Vodacom na CCBRT, mwaka huu pia alizunguka kwenye mikoa kadhaa nchini kwenye kampeni ya Fistula na alikuwa msemaji. Kama hip hop ingekuwa uhuni, sidhani kama Vodacom wangempa heshima hiyo.

Roma Mkatoliki
roma
Mashairi ya Roma hayapishani sana na makala za mwandishi kama Said Kubeneya wa gazeti la Mwana Halisi. Tofauti ni moja tu kuwa ujumbe wa Roma huwasilishwa kwa njia ya muziki. Tangu ameanza, nyimbo zake nyingi zimekuwa zikigusa maisha na matatizo ya wananchi wa Tanzania na pia kukemea maovu ya mafisadi na viongozi wabovu. Sidhani kama mtetezi kama huyu anaweza kuitwa mhuni…

Kala Jeremiah
1238824_729781967048150_784816076_n
Kutoka Mwanza kwenye mitumba, hadi kuwa balozi wa Pepsi. Nyimbo nyingi za Kala zimekuwa zikigusa maisha halisi ya Mtanzania na ndio maana alifanikiwa kuwashawishi watu wa Pepsi. Kuanzia Wimbo wa Taifa, Ningekuwa Rais, Dear God, Jaribu Kujiuliza na zingine.
“Ni hatua kubwa na jinsi gani sasa muziki wetu wa Hiphop unaeleweka vizuri. Kama hip hop inaweza kushawishi makampuni kama hayo kuwekeza nadhani inaeleweka,” Kala aliiambia Bongo5 baada ya kupewa ubalozi wa Pepsi.

Source: Bongo5

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname