14 November 2013

HAYA NDIO MAISHA...!LADY JAYDEE 'ANACONDA' SASA YUPO MBIONI KUFUNGUA RADIO STATION YAKE.....!!


Nimeshangaa sana baada ya kuona AWARDS mbalimbali alizojinyakulia LADY JAYDEE tokea aanze muziki apa bongo mwaka 2000 hadi sasa 2013,tokea mwaka huo(2000) aanze muziki alibahatika kujinyakulia tunzo na hadi leo hii hajawahi kukosa tunzo ukijumlisha na zile alizopata Uganda kama mara nne au tano.

Hivi,tokea aanze muziki mwaka huo JIDE hajawahi kuchuja hadi leo hii bado yupo juu kimuziki hata kimaisha,kumbuka ni miaka kumi na tatu (13) sasa.Ki ukweli huyu msanii anahitaji heshima ya kipekee apa bongo na nchi za jirani pia.Hiki kitu sio cha kawaida kabisa kuwahi kutokea apa bongo.

Achilia mbali mafanikio aliyoyapata ya kujenga jumba la kifahari,kumiliki mgahawa wa kisasa (NYUMBANI LOUNGE),kumiliki band ya music,kufungua STUDIO YA MUZIKI,na hivi karibuni yupo njiani kufungua RADIO STATION yake binafsi,can u imagine???,kufungua radio station sio kitu cha kawaida hata kidog especially kwa wasanii wetu wa apa bongo.Kwa sasa HAKUNA msanii yeyote awe wa kike au wa kiume mwenye ubavu wa kushindana na huyu bidada,SHE IS THE NUMBER ONE.
Kama ulikuwa hujui huyu ndiyo KOMANDO na huu ndiyo UCHAWI ambao msanii yeyote wa bongo mwingine hajaweza kufanya..!!

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname