MWIGIZAJI wa Filamu Bongo Dianarose kimaro ‘Diana’ ametamba kwa kusema kuwa amekamilika katika tasnia ya filamu na hakuna mwigizaji wa kike ambaye anamfikia kwa kiwango alicho nacho katika uigizaji kwani kila akiwangalia wanaigiza kawaida na hajaona mpinzani wake wa kweli katika fani hiyo Swahiliwood kwa sasa.
.
“Nilipokuwa shule nilijitenga na sanaa sasa nimerudi watasubiri kwa upande wa wasanii wa kike wanaigiza kwa kiwango cha chini, au kwa kutopewa nafasi wanazomudu kuna watu wanajua mimi na Lulu ni mapacha lakini kwa filamu niliyoifanya hivi karibuni ya Kigodoro shoga yangu atasubiri,”anasema Diana.
Diana ambaye mara nyingi ushirikiana na Lulu kataika filamu kwenye uigizaji sasa anasema ameamua kusimama yeye kama yeye na anawahakikishia kuwa wapenzi wa filamu kuwa wasubiri filamu inayokuja ya ‘Kigodoro Kanitangaze’ambayo kaigiza kama mhusika akitamba kuwa yeye ni kiboko yao rika lake lote anawafunika.
No comments:
Post a Comment