Rapper wa kampuni ya Weusi, Nick wa Pili amefanikiwa kuhitimu shahada yake ya pili kwenye chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM.
Nick aliitoa taarifa hiyo kwenye kipindi cha Club 10 cha Clouds FM na kutoa ushauri kwa wanafunzi wanaofanya muziki.
“Mimi ni mwanafunzi, jana nimemaliza degree ya pili mlimani. Nimefurahi kuna wanafunzi wanataka kuwa kama mimi,kuna vitu vichache vya msingi vya kuzingatia kwa upande wa sanaa. Inabidi waache mambo mengi ya sanaa wachague kitu kimoja, atake kuwa msanii bora. Ukitaka kuwa msanii bora usihangaikie mambo ya kwenda studio, sijui kumtafuta nani ,sijui kutafuta interview, atake kuwa msanii..
No comments:
Post a Comment