Kufuatia habari iliyotoka
juzi baada ya kuandikwa na gazeti moja la udaku na baadaye kusambaa
mitandaoni kuwa muigizaji maarufu nchini Wastara Juma Sajuki anafikiria
kuolewa ikiwa ni takribani mwaka na miezi kadhaa tangu aliyekuwa mume
wake na star wa filamu pia Juma Kilowoko(Sajuki) kufariki dunia,
muigizaji huyo amefunguka ya moyoni mwake kupitia page yake ya facebook
akionekana hana mpango wa kuolewa leo au kesho bali Sajuki bado yupo
moyoni mwake. Star huyo wa filamu za Vivian, Mboni Yangu, Kivuli na Vita
aliandika hivi jana katika page yake "Milele uko ndani ya moyo.wangu
kokote niendako nipo nawe ni kazi sana kuziba pengo langu, nakupenda ni
wewe tu
Haupo kimwili lakini umeondoka na umeondoka na nusu ya akili yangu huku
hakuna linalofanyika bila kuvuta taswira yako nakupenda sana Sajuki"
No comments:
Post a Comment