BAADA ya shoo ya Tamasha la Serengeti
Fiesta 2013 jijini Dar kusimama kwa muda leo alfajiri kwa hitilafu ya
umeme, itandelea tena saa 9 alasiri leo katika Viwanja vya Leaders
jijini Dar es Salaam bila kiingilio.
Akizungumza na baadhi ya mashabiki wa
tamasha hilo waliokuwepo viwanjani hapo baada ya hitilafu kurekebishwa,
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa
Clouds Media Group, Ruge
Mutahaba alisema kuwa shoo itaendelea saa 9 na wasanii Nasibu Abdul
'Diamond Platnumz' Davido kutoka Nigeria, Mohombi kutoka Sweden, Nay wa
Mitego na Bendi ya Twanga Pepeta watatoa burudani ya nguvu.
Aliongeza kuwa mashabiki wategemee
'sapraiz' kibao wakati wa shoo hiyo. Wasanii waliopiga shoo baada ya
umeme kurudi katika hali yake ni pamoja na Kalapina, Chid Benz na Darasa
japo mashabiki wengi walikuwa wameondoka viwanjani hapo
No comments:
Post a Comment