JUMA Nature amedai kuwa wasanii wengi
wamemuiga, Mb Doggy na kusababisha muziki wa Bongo Fleva kupoteza
mwelekeo kwa vile hawataki kufikiria kufanya kazi tofauti.
Nature amesema muziki wa zamani ulikuwa na mafanikio kwa kuwa wasanii walikuwa wakiimba kwa staili tofauti.
“Huko nyuma tulifanya muziki wenye ladha
zinazotofautiana, kila mtu alijitahidi kufanya kazi yenye utofauti.
Staili hii ya sasa maarufu ya kubana pua alikuja nayo Mb Doggy na kwa
kweli nilifurahi kwani alikuwa amefanya kitu chenye utofauti,” alisema.
“Lakini hali ni tofauti hakuna aliyekuja
na wazo lingine, wote bado wapo palepale. Ni vyema tukajifunza ubunifu
ili sanaa yetu isonge mbele.”
Alitoa ushauri kwa wasanii wa sasa kuwa
wangeacha kuimba nyimbo za mapenzi na badala yake wageukie jamii ili
kuweza kutoa elimu katika nyanja mbalimbali.
“Nikipanda jukwaani naimba nyimbo zangu
za mwaka 2000 hadi 2012 lakini zote ni kama ndiyo kwanza nimezitoa, ni
kwa namna mashabiki wanavyozipenda,” alisema Nature (pichani).
Alipoulizwa kuhusu hilo, Mb Doggy
alisema: “Ubunifu wangu ulikuwa mzuri, namshukuru Mungu nilibuni kitu
kinachoishi ila si kwamba nimeua Bongo Fleva. Kilichopo ni kwamba vijana
wa sasa wapanue mawazo ili waje na kitu bora zaidi, ni kweli kuwa kila
mtu sasa anaimba kama mwenzake.”
No comments:
Post a Comment