Kwa mujibu wa Kamanda, Lukumay alimuuzia dawa za miti shamba mteja wake kisha kuzinywa na alifariki muda mfupi baadaye.
Hata hivyo haikufahamika ugonjwa uliokuwa ukimsumbua.
“Lukumay anauza dawa za asili ya Kimasai, ambazo ni baadhi ya mitishamba na vitu vingine, inadaiwa siku ya tukio alimpa dawa mteja wake huyo ambaye uchunguzi wa awali unaonesha alifariki baadaye, tunamhoji kujua chanzo cha kifo,”alisema.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa ya Mawenzi. Polisi inafuatilia kufahamu iwapo dawa za mtuhumiwa huyo zinatambuliwa na mamlaka zilizopo na kama anatambulika kuendesha biashara anaifanya kienyeji.
Pamoja na tukio hilo la kifo, pia polisi imetoa taarifa juu ya mtoto mchanga wa kike anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miezi sita na saba aliyekutwa amekufa akiwa katika dampo lililopo Kata ya Njoro, Manispaa ya Moshi. Polisi imeomba wananchi kushirikiana na polisi kubaini wahusika wa tukio hilo
No comments:
Post a Comment