Baada ya biashara ya wizi wa kutumia mitandao kupungua, wengi wasio na
kazi, wenye stress and vijana wa Kinigeria wenye malengo makubwa kupita
uwezo wao hasa hasa wale wanaopenda maisha ya kutajirika haraka
wameingia kwenye biashara mbaya zaidi ya kujipatia pesa kwa kuza figo
zao. Kwa uchumi unaondelea kudoroa and idadi kubwa ya watu wasio na
ajira nchini humo, hii biashara, ingawa ni ya zamani kwa sasa ndio
inashika kasi.Alhamisi ya tarehe 18 Aprili ya mwaka 2013 kijana aitwae Kingsley
Odoh mhitimu wa Institute of Management and Technologia (IMT) pale Enugu
arudi inchi kwao Nigeria kutodea Malaysia. Ghafla tu baada ya kuingia
nchini kwake kwa mbwembwe nyingi katika kituo cha ndege cha Akanu Ibiam
hapa Engu, hali ya hewa kwake ilikuwa imebadilika. Ukiachana na
muonekano wake wa kitajiri, aliwaalika marafiki zake wa muda mrefu kwa
kuwapatia vinywaji aina ya wine katika hoteli ya gharama zaidi hapa
Nigeria iitwayo Protea.
Ilidhaniwa kuwa labda alipata pesa za muda tu lakini wiki zimepita na
mpaka leo makazi ya Odoh yapo sehemu inaitwa Independence Layout hapa
Enugu na hiyo sehemu yake sasa inaonekana kama mbingu ya starehe za wine
na vyakula. Marafiki wapya na wazamani wanafurika kwake kupata wine na
vyakula.
Ukiachia mbali kwa yeye kuhama chumba chake alichokuwa anaishi chuoni
kwao ambako walikuwa wanaishi wane wane Odoh anazunguka tu mjini
akisukuma mkoko Sports wenye gharama balaa, na kampani yake ni wasichana
wazuri wa aina yoyote atakayo yeye na wengi wao ni wanafunzi wa IMT au
ESUT. Wakati watu wengi wakijiuliza ni nini amefanya Odoh kilichomfanya
awe tajiri ghafla watu wengine wa karibu wanajua kuwa pesa hizo
hazitokani na wizi wa kwenye mitandao bali aliuza figo yake mwenyewe
alipoenda nchini Malaysia.
“Kama utapenda nitakuunganisha kwa wahusika. Ukweli ni kwamba hakuna
kosa kwa kile nlichokifanya. Kama watu wanaweza kujitolea figo zao bure
na kuokoa maisha ya wengine, kwanini mtu mwingine asitumie figo yake
kuokoa maisha ya wengine na vilevile kujipatia pesa ambayo itamkwamua
kutoka kwenye umasikini. Hiko ndio nilichofanya na sijilaumi” aliliambia
Sunday Express.
Odoh akaendelea kurusha kombora: “Sasa hivi navyoongea na wewe, kuna
Wanigeria wengi sana wako kwenye foleni nchini Malaysia ambao tayari
wameshafanya utaratibu wa kuuza figo zao. Wengine wanashauku ya kupata
hela ili kuanzisha vitu ambavyo vitaendesha maisha yao. Siwezi kusema
wote wanaziuza lakini ukweli ni kwamba hata wale ambao wachagua
kuzichangia bure bado wanapewa pesa za kufutia jasho. Kwahiyo tofauti
iko wapi?” alisema Odoh. Story Ya Odoh inaendelea kwa<<BOFYA HAPA INAENDELEA KWA KIINGEREZA>>
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI..
No comments:
Post a Comment