Bwana Reginard Mengi ameonesha
kusikitishwa na kauli ya Waziri wa madini Prof Sospeter Muhongo kwa
kusema kuwa Watanzania hawawezi kuwekeza kwenye gesi na badala yake
wafanye biashara ya kuuza juice.
Akihojiwa leo NA SAUTI YA AMERIKA,
Mengi amesema kuwa kwanza serikali kugawa gesi kwa wageni bila hata
kuwepo kwa sera ya gesi ni uporaji mkubwa wa mali za Watanzania bila
ridhaa yao. Amemwambia hayo maneno ya kuuza juice
aende akawaambie
wanafunzi wake na asidhani kila Mtanzania hawezi kuwekeza kwenye gesi.
Amemshauri arudi chuo akafundishe na maswala ya gesi awaachie Watanzania
Source:SAUTI YA AMERIKA

No comments:
Post a Comment