Vicky Kamatta akichunga mbuzi.
Akiwa na kundi la wanyama hao wapatao 27 huku akionekana mwenye
dalili za uchovu, mheshimiwa huyo alikutwa maeneo ya Kibamba, nje
kidogo ya jiji ambako aliweka wazi kuwa kuchunga ni sehemu ya maisha
aliyopitia.“Hili ni shamba langu na hawa ni mbuzi wangu, kazi ya kufuga, siyo Mbuzi tu hata wanyama wengine ni asili yetu kule usukumani, siwezi kuikacha kwa kisingizio cha ubunge,” alisema Vicky ambaye kabla hajawa mbunge, aliwahi kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya.
“Hii ni kazi ambayo nimekua nikiifanya huko nyumbani (Geita), hivyo hata kwa sasa ninapopata nafasi kama hii, hasa mwishoni mwa wiki, huja huku kujikumbushia maisha yangu ya zamani.”
Alisema fikra za wengi kuwa wanasiasa huishi tofauti na wananchi wa kawaida siyo kweli, kwani wengi wao wametoka katika maisha ya kawaida kabisa vijijini.
Akiwa msanii, Kamatta alitamba na kibao chake kisemacho Wanawake na Maendeleo.
No comments:
Post a Comment