Westgate Mall kabla ya shambulio la magaidi
NAIROBI, Kenya
Serikali ya Kenya imeilaumu Serikali ya Marekani kwa kuwaonya
raia wake wasisafiri kwenda nchini humo kutokana na shambulizi la
Septemba 21 mwaka huu, katika jengo la biashara la Westgate, jijini
Nairobi, nchini humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Kenya, Bw. Joseph Ole Lenku, alitoa
lawama hizo jana kwa waandishi wa habari wakati akizungumzia uchunguzi
wa Serikali juu ya shambulizi hilo linalodaiwa kufanywa na wanamgambo wa
Al Shabaab.
Bw. Lenku alisema kuwa, tahadhari hiyo kwa raia wa Marekani si ya kirafiki na Kenya ingawa uchunguzi huo, ulikuwa ukifanywa na polisi wa nchi hiyo, makachero wa Israel, Marekani na Ulaya.
Alipinga na kulaani ushauri wa Marekani kwa raia wake na kuwataka wathamini hali ya usalama wao binafsi kutokana na vitisho vya kigaidi vinavyoendelea na vya hivi karibuni katika Taifa hilo la Afrika Mashariki.
Ingawa hakuitaja moja kwa moja sekta ya utalii, maelezo ya Bw. Lenku yanaonekana kuhofia biashara hiyo nchini humo jinsi inavyoweza kuathirika katika kipindi hiki kwani sekta hiyo inaingiza dola za Marekani bilioni moja kila mwaka.
“Tumesikitishwa na ushauri huo ambao haukustahili, hauna umuhimu na si urafiki…unapingana na mapambano dhidi ya ugaidi wa kimataifa,” alisema Bw. Lenku.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Reuters la Uingereza, mbali na wahanga 50 wa Kenya, raia kutoka Uingereza, Ufaransa, China, Ghana, Canada, Australia, Afrika Kusini, Peru na Uholanzi pia waliuawa katika shambulizi hilo la kigaidi

Majira
No comments:
Post a Comment