07 October 2013

JE NI KWELI CLOUDS TV WANA COPY VIPINDI KUTOKA EATV?

Ubunifu ni kitu pekee kinachoweza kuitofautisha brand moja hadi nyingine/kampuni nyingine ambazo/yo inatoa huduma zinazolingana/fanana.

Nirudi kwenye topic,sina shaka na uwezo wa clouds media Group katika ubunifu na mambo mengine linapokuja suala la burudani hapa Tanzania, ila kwa hili niseme Clouds TV wamekosa ubunifu na walichoishia kufanya ni kukopy na kupaste vipindi vyao kutoka TV stations nyingine mfano EATV.Vifuatavyo ni baadhi ya vipindi ambavyo Clouds TV wamekopy na kupaste kutoka EATV....

1.Siz kitaa- City sound (kilichokuwa kikiendeshwa na Seki)

2.Take One-Bongo movie (kilichokuwa kinaendeshwa na Joyce Kiria).

3.Ongea na Janeth-The Mboni show (kinachoendeshwa na Mboni)

4.Wazee wa Madebe-Friday Night Live(kinachoendeshwa na Sam Misago).

5.kipindi cha Paradise cha Irene uwoya nayo ni programu ambayo inendeshwa na TV stesheni nyingi za nje katika mtindo wa documentary,lakini kipindi hiko kinafanana kabisa na kipindi ambacho hufanywa huko Nigeria na moja ya TV stesheni,so sio kitu kipya pia.


Mdau unaweza kuongeza vipindi unavyovijua ambavyo jamaa wamecopy ila si kwa nia mbaya.

Source:Jamii Forums

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname