WACHUMBA wa zamani, Wema Sepetu na
Nasibu Abdul ‘Diamond’ ndiyo habari ya mjini kwa sasa, kwamba wawili hao
wamerudiana tena kwa kasi kupita ile ya mwanzo, Amani limechimbua.
Habari zinasema wawili hao walikutana
Dubai hivi karibuni kabla Diamond hajaenda Malaysia na Wema akiwa
njiani kuelekea Hong Kong, China ambapo walikula bata kwa sana.
Ikazidi kuelezwa kuwa wameamua kuwa
kwenye uhusiano wa siri na lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha mpenzi
wa sasa wa msanii huyo wa Bongo Fleva, Penniel Mungilwa ‘Penny’ hajui
kitu chochote.
TAARIFA ILIVYO
Kwa muda wa siku nne, ndani ya mitandao
ya kijamii hasa kwenye Instagram, maneno yenye kuashiria kuwa wawili hao
wapo pamoja tena yamekuwa yakichukua nafasi.
Baada ya kusambaa kwa habari hizo, Penny
naye alitupia picha yake akiwa kitandani na Diamond na kuandika kuwa
waachwe kama walivyo.
Ndani ya mtandao wa Instagram yakazuka
makundi mawili, upande wa mawifi wa Penny, akiwemo Halima Kimwana na
kundi lingine la mawifi wa upande wa Wema.
Kundi la Wema waliandika kuwa mwanamke
anayependwa na ndugu wa mume siku zote mwanamme huwa hampendi hivyo Wema
ni mpenzi sahihi wa Diamond kwa vile hapendwi na ndugu kama Penny.
MBAYA ZAIDI
Mbaya zaidi, katika hali isiyotegemewa
kwenye akaunti yake ya Instagram, Wema alitupia wimbo mpya wa Diamond
uitwao My Number One na kuweka maoni yake kwamba anaupenda wimbo huo.
Wengine waliochangia walisema Wema ana
lake jambo kwa Penny kwa vile si jambo jepesi kusifia wimbo wa mwanamme
ambaye alikuwa mpenzi wake na sasa ana mwingine anayejulikana, yaani
Penny.
PICHA YA WEMA SASA
Wema hakuishia kuposti wimbo huo tu,
alikwenda mbele zaidi kwa kutupia picha yake yenye pozi tamu na kuuliza;
huyu hapa baby wa nani huyu? (yaani yeye).
Wengi walimsifia lakini wengine walifunguka kwa kusema ni baby wa Diamond, jambo ambalo Wema hakulipinga.
PENNY AONGEA NA AMANI
Kufuatia kuenea kwa habari hizo, Amani
lilianza kuwasaka watu watatu ambao ndiyo wenye uwezo wa kubainisha
ukweli au uongo wa ishu hiyo iliyoenea mjini.
Watu hao ni Diamond mwenyewe, Wema anayedaiwa kurudiwa na Penny, mpenzi wa sasa wa Diamond.
Wa kwanza kupatikana alikuwa Penny ambapo alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa madai hayo alifunguka:
AKIRI KUNYETISHIWA
“Ni kweli hata mimi nimenyetishiwa habari hizo lakini siamini kama inawezekana hao watu wakarudiana.
ASEMA KUNA KUNDI LINAPANGA NJAMA
“Nijuavyo mimi kuna kundi la watu ambao
wapo upande wa pili (wa Wema) ndiyo wanaoeneza hizo habari, pengine
wanataka niamini kisha nimwache Diamond, simuachi ng’o.
ANATAKA USHAHIDI
WA PICHA
“Kama niliweza kumvumilia kwa kuona picha akiwa na Irene Uwoya hotelini sembuse hili la safari hii hata picha hakuna?”
ALISHAMUULIZA DIAMOND
“Mimi nilishamuuliza Diamond, japo hakusema ni kweli au uongo ila aliniambia achana na hizo habari.”
DIAMOND APIGA KIMYA
Baada ya kuongea na Penny,
lilimpigia simu Diamond ambapo alipokea
na kusema yuko kikaoni na kumtaka paparazi kupiga baadaye. Hiyo ilikuwa
saa 4:16 asubuhi ya juzi.
Saa 7:11 mchana, Diamond alipigiwa simu
tena lakini hakupokea. Akatumiwa meseji ya kumkumbushia, hakujibu.
Akatumiwa meseji yenye madai ambayo pia hakuijibu.
MAMA WEMA KABLA YA KUULIZWA AFUNGUKIA MADAWA YA KULEVYA
Amani liligundua Wema bado yupo Hong
Kong hivyo liliamua kumpigia simu mama yake, Bi. Miriam Sepetu ili
kuomba namba ya bintiye, lakini kabla ya ombi hali ikawa hivi:
“We nani, hivi kuna gazeti moja
limeandika eti mwanangu amekamatwa na madawa ya kulevya China anasubiri
kunyongwa, ni akina nani wale, wana akili kweli?
“Mimi sikubali safari hii, tutafikishana kwa mwanasheria wangu.
“Tena ukikutana nao waambie waache kumzushia mwanangu, wasimtie mkosi bure, hajakamatwa yupo salama kabisa.”
Mpaka sasa ushahidi wa kuonesha wapenzi hao wa zamani kuwa wamerudiana bado haujawekwa hadharani.
GPL
No comments:
Post a Comment