BREAKING NEWS: VURUGU ZATOKEA MBAGALA, BARABARA YAFUNGWA..BAADA YA MWANAFUNZI KUGONGWA NA GARI NA KUFA
-Ni baada ya mtoto kugongwa na gari
-Barabara imefungwa kuanzia saa nne asubuhi
-Umati mkubwa wakusanyika eneo la tukio
KUNA vurugu zinaendelea eneo la Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam
na wanachi wamefunga barabara baada ya mtoto kugongwa na lori na
kupoteza maisha. Vurugu hizo zimeanza saa nne asubuhi baada ya ajali
hiyo na mpaka sasa zinaendelea. Polisi wamefika eneo la tukio kujaribu
kuzuia vurugu hizo lakini wameshindwa maana watu ni wengi. Kwa sasa
hakuna gari lolote linalopita katika eneo hilo na baadhi ya wananchi
wanachoma matairi. Habari zaidi, zitawajia baadaye
No comments:
Post a Comment