Siku chache zilizopita mwana Hip Hop kutoka pande za Manzese Nay Wa
Mitego alipokea barua kutoka BASATA inayomtaka kubadili aina ya mavazi
anayovaa katika show zake (mlegezo/mtepesho) ambayo hayaendani na
Tamaduni za kitanzania.
Akizungumza na Bongo5 leo kwa njia ya simu Nay amesema amekuwa akivaa
mlegezo kwa kipindi cha miaka ishirini hali ambayo itamwia vigumu
kubadilika kutokana ni mtindo ambao ata mashabiki wake wengi wameuzoea.
“Nahisi kuna kitu kingine wanakitaka toka kwangu kuhusu muziki
wangu ndiyo maana wananitishia kunifungia wakati mimi nafanya muziki
kama ndiyo maisha yangu, kwahiyo kubadilika kwa haraka kuvaa mlegezo
siwezi labda baada ya miaka 3 ila inategemea” Alisema Nay.
Aidha katika mahojiano mengine na kipindi cha Showtime kupitia kituo
cha RFA ya Mwanza Nay amesema kuwa Baraza hilo lina majukumu mengi ya
kufanya kwaajili ya kuboresha maslahi ya wasanii badala ya kuhangaika
na kumzuia kuvaa mlege ili hali wanaovaa hivyo ni wengi.
“Sasa hata baraza la sanaa Tanzania wana shughuli nyingi sana za
kufanya nyingi sana ili sanaa yetu isonge mbele mambo yetu yaani
wasanii tuishi maisha mazuri lakini si swala la kufuatilia mlege wa Nay,
hapana kuna kitu behind ambacho kinaendelea sijui ni nini maybe
wameamua waanzie hapo ili wastopishe kile ambacho nakifanya.”
Source: Bongo5
Source: Bongo5
No comments:
Post a Comment