TAARIFA YA
NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA,
UTAMADUNI NA
MICHEZO, MH. AMOS MAKALLA
KWA VYOMBO VYA
HABARI
Napenda
kuufahamisha umma kwamba mimi ndiye NILIYERUHUSU Gazeti la Mwananchi kuendelea
na utoaji wa taarifa/habari kwenye tovuti yake, pia Gazeti la Rai kutoka kila
siku.
Ninalazimika kutoa
ufafanuzi kwa njia ya maandishi kutokana na kupigiwa simu nyingi na waandishi
wa habari kuhusiana na tamko jipya la Mkurugenzi wa Habari – Maelezo, Ndg Assah
Mwambene kuhoji uhalali wa Gazeti la Mwananchi kuwa online na Gazeti la Rai
kutoka kila siku, badala ya mara moja kwa wiki (Alhamisi).
Tarehe 4/10/2013
nilifanya mazungumzo na viongozi wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd
(MCL) na New Habari Corporation (2006) Ltd kwa upande mmoja na msajili wa
magazeti kwa upande mwingine.
Katika kikao hicho
cha pamoja na viongozi wa Magazeti ya Mwananchi na Mtanzania maombi matatu
yaliwasilishwa;
1. Ombi la kumuomba
waziri apitie upya adhabu iliyotolewa kwa mageazeti hayo. Katika hili Majibu
yangu niliwaambia kwamba mwenye mamlaka juu ya suala hilo ni waziri mwenye
dhamana na masuala ya habari pekee.
2. Ombi la Gazeti
la Mwananchi kuwa online na Gazeti la Rai kutoka kila siku badala ya kutoka
siku ya Alhamis.
2.1 New Habari
walieleza kuwa siku zilizopita waliwahi kuomba kwa maandishi (barua) kwamba
gazeti la Rai litoke kila siku. Maelezo ya Naibu Msajili wa Magazeti katika
kikao hicho yalikuwa kwamba, kulikuwa na tatizo la kiufundi katika kurejea
maombi hayo na akakiri kuwa hakuna kinachozuia gazeti la Rai kutoka kila siku.
Kutokana na maelezo hayo mimi niliridhia gazeti hilo sasa liruhusiwe kutoka
kila siku.
2.2 Kuhusu gazeti
la Mwananchi kuwa online, Naibu Msajili alisema hakuna sheria yeyote inayoweza
kuzuia gazeti hilo kuwa online
ila aliwataka
lisionekane gazeti zima kama lilivyo pia wabadili nembo (Master Head) kwamba
waweke nembo ya MCL na siyo ya gazeti husika ambalo limefungiwa. Pia baada ya
maelezo hayo niliridhia gazeti hilo liwe mtandaoni kwa kuzingatia angalizo
lililotolewa na Naibu Msajili wa Magazeti.
3. Hoja ya tatu
ilikuwa ni ile ya Serikali kupitia Idara ya Habari - Maelezo kuwa na uhusiano
mzuri na vyombo vya habari, ili kuepuka misuguano isiyo ya lazima.
3.1 Pendekezo hili
nililipokea na niliwasilisha kwa Mhe Waziri wa Habari kwa hatua zaidi, likiwamo
suala la kupitia upya adhabu na ushauri wa kujenga uhisiano na vyombo vya
habari.
3.2 Masuala ya
Gazeti la Mwananchi kuwa online na Rai kutoka kila siku, NILILITOLEA UAMUZI
siku hiyo hiyo, na uamuzi ni kwamba niliwaruhusu baada ya kuridhika kwamba
hakukuwa na ukiukwaji wa sheria yoyote uliofanywa na waombaji.
Nimeamua kuweka
sawa jambo hili kutokana na taarifa ya Mkurugenzi wa Maelezo ambayo ninaamini
kwamba kutolewa na kusambazwa kwake ni kukosekana kwa mawasiliano kati yake kwa
uipande mmoja na Mhe. Waziri, Naibu waziri na Naibu Msajili wa Magazeti kwa
upande mwingine.
Hivyo aliyeruhusu
Gazeti la Mwananchi kuwa online na Rai ni mimi na ndiyo maana kuanzia tarehe
5/10/2013 Gazeti la Rai lilianza kuchapwa kila siku na kusambazwa, na Gazeti la
Mwananchi likaanza kuwa mtandaoni kwa kuzingatia maelekezo ya Naibu Msajili wa
Magazeti.
Imetolewa na:
Amos G. Makalla
Naibu Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
11 Oktoba 2013
No comments:
Post a Comment