"SIPIMWI UKIMWI NG'OO"....JOHARI
STAA wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa
hana mpango wa kupima ‘ngoma’ kama ilivyoripotiwa katika baadhi ya
vyombo vya habari.
Akiongea na paparazi wetu, Johari alisema hakufurahishwa sana na
taarifa hizo za kupima ugonjwa huo na kusema ukweli ni kwamba yeye
hajawahi na wala hana mpango wa kupima.
“Nachukia sana watu kusema kuwa eti tunapimisha watu Ukimwi, nahisi
kuna mtu anataka kunichafulia tu. Sisi wote hapa RJ hatujapima Ukimwi
wala hatuna mpango wa kufanya hivyo,” alisema Johari.
No comments:
Post a Comment