Msanii zilipendwa kwenye sanaa ya filamu
Sintah amefanya madudu mengine baada ya kuandika habari ya uongozi na
uchochezi na kukipakazia kituo cha redio time fm cha Jijini Dar kuwa
kilishindwa kujipanga kwenye shoo yao iliyofanyika mwishoni mwa juma
kwenye suala la ulinzi hadi kupelekea wasichana kubakwa na kuporwa mali
zao.
Habari hiyo iliwashangaza waandaji wa
tamasha hilo pamoja na jeshi la polisi Kanda ya Kinondoni ambalo
lilikuwepo uwanjani usiku kucha wakingozwa na mkuu wa kituo cha Polisi
Oysterbay Wilbrod Mtafungwa hadi asubuhi bila kushuhudia matukio
mabaya.
Katika habari hiyo ya Sintah iliyokuwa
inasema kuwa Wasichana wabakwa usiku kucha na wahuni kwenye shoo ya
Azonto bila msadaa wowote jambo ambalo Jeshi la Polisi Kinondoni
limekanusha vikali madai hayo huku ikisema kuwa hadi leo Jumanne hakuna
taarifa yoyote kuhusiana na madai hayo ya Sintah.
Akiongea mmoja wa askari wa kituo cha
Oysterbay ambae aligoma kutaja jina lake kwa madai kuwa yeye si msemaji
alisema" Tumeshangazwa sana na taarifa ya Sintah aliyoiandika jana
Jumatatu mapema kuwa kuna wasichana walibakwa usiku kucha hii habari
naona ilikuwa na mlengwa wa kushoto kwa kuchafuliana habari hiyo haina
ukweli wowote kwani hadi sasa sisi kama Polisi tuliopewa jukumu la
kulinda wananchi ziku zile hatuna taarifa hizo" Alisema afande huyo
Hata hivyo jeshi hilo lilikuwa na mpango
wa kuhitaji ushahidi wa vielelezo juu ya habari hiyo ambavyo Sintah
angetakiwa kuviwakilisha polisi ili waweze kuwasaka wabakaji hao
vinginevyo habari hiyo ingemletea matatizo Sintah kwani ni ya uchochezi
na unafiki.
Siku ya shoo hiyo ya mwanamuziki Azonto
toka nchini Ghana mwenye makazi yake nchini Uingereza ilikuwa na ulinzi
mkali sana kulikuwa na Mbwa wa polisi 15, Polisi wasiopungua 90
wakiwemo wale wenye siraha ambao walikuwa wanazunguka viunga vya uwanja
wa Ustawi wa Jamii.
Aidha baadhi ya mashabiki wengi walisema
kuwa huenda Sintah bado ana hasira na kituo hicho cha redio times baada
ya kupigwa chini kwenye kipindi alichokuwa anatangaza kutokana na
kukosa sifa ya kuendesha kipindi hali iliyosababisha Sintah kuwawekea
bifu.
Hata hivyo Sintah aliitoa haraka habari
hiyo kwenye blog hiyo baada ya kutonywa na wasamalia wema kuwa
ingemletea matatizo makubwa kwani kama hana ushahidi wa vielelezo ni
heri akaitoa na mara moja alifanya hivyo.
Xdeejayz iliwasiliana na uongozi wa
redio times lakini bahati mbaya simu zao zote zilikuwa bize kila
walipopigiwa simu, hata hivyo tunawaahidi wasomaji wetu kuwa itamtafuta
mkurugenzi wa kituo hivho Rehure Nyaulawa kuzungumzia suala hilo na kama
kuna hatua zozote wameshaanza kuzichukua juu ya Blog hiyo kwa kuandika
bahari hiyo ya uongo.
No comments:
Post a Comment