01 September 2013

SIMUAMINI TENA MKE WANGU...NIMFANYAJE MKE WA NAMNA HII?

Mimi na wife tumebahatika kupata watoto 2 wa kiume! Mm nafanya kazi dsm yy anafanyia mara. kijana wetu yupo grade 1 kwenye hizi academy! Takriban wiki kadhaa nilienda kumsabahi! Nije kwenye pt niligundua amekuwa akiwatumia ndg zake pesa nyingi paspo kunijulisha nahc kuna business wanafanya yy na
dadake! Niligundua baada ya kumwambia kwamba mm kulingana na ujio wangu siko fresh kiuchumi hivo jitahidi ada ya mtoto make ndo wanafungua mwezi wa tisa kwa kifupi alinipa majibu ya kunikatisha tamaa akadai hana hela na isitoshe kwenye ubini wa mtoto anaandikwa yy au mm? Km sitaki kumsomesha akae nyumbani! Nikamuuliza km waweza tumia ndg zako malaki ya pesa unashimdwa nn kumlipia mwanao? Akakanusha wakati mm nilicheki kwenye mpesa ametuma pesa two times tena last month! Tukazinguana sana mm nikapanda basi nikasepa kwa ufupi hana mpango wa kusaidiana na mm ktk kusukuma gurudumu! Nimfanyaje mke wa namna hii?

Source:JF

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname