THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S
OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O.
BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Obama amimina pongezi kwa Tanzania
·
Amkumbatia
Rais Kikwete akimwita “kaka na rafiki”
Rais
wa Marekani Mheshimiwa Barack Obama ametoa pongezi na sifa kwa Tanzania kwa
kuwa miongoni mwa nchi chache duniani ambazo zimetia saini mkataba wa
Ushirikiano wa Serikali Zinazoendeshwa kwa Uwazi ambao unalenga kujenga na
kuendeleza nafasi ya taasisi zisizokuwa za Kiserikali katika utawala bora,
uwazi na uwajibikaji katika uendeshaji wa Serikali.
Rais
Obama ametoa pongezi hizo kwa Tanzania leo, Jumatatu, Septemba 23, 2013, wakati
akizungumza katika mkutano maalum aliouandaa mwenyewe Rais Obama kuzungumzia
nafasi za Serikali katika kuunga mkono na kuendeleza asasi na taasisi
zisizokuwa za Kiserikali na kuzishirikisha zaidi katika kuboresha shughuli za
utawala bora uliofanyika kwenye Hoteli ya Hilton, mjini New York, Marekani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa
miongoni mwa viongozi wachache duniani walioalikwa kushiriki mkutano huo maalum
ambao pia ulishirikisha wawakilishi wa asasi zisizokuwa za Kiserikali 300.
Baadhi
ya nchi nyingine za Afrika zilizoalikwa na kushiriki katika mkutano huo ni
pamoja na Liberia, Ghana, Benin, Libya, Tunisia, Senegal, Afrika Kusini na
Botswana.
Shabaha
kuu ya mkutano huo wa saa moja ilikuwa ni kutafuta namna ya kuongeza kiwango
cha kuungwa mkono kwa taasisi na asasi hizo na jinsi gani ya kuzilinda ili
kuziwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Aidha,
mkutano huo ulilenga kuzitaka Serikali ambazo zinaweka vikwazo kwenye utendaji
wa asasi hizo kuondoa vikwazo hivyo haraka ambavyo vinahujumu utendaji kazi na mchango
wa asasi hizo katika uendeshaji wa utawala bora.
Katika
hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Rais Obama amezisifia nchi kama
Tanzania ambazo zimetia saini makubaliano ya Ushirikiano wa Serikali Wazi
ambayo yanalenga kupandisha nafasi ya asasi zisizokuwa za Kiserikali katika
Utawala Bora,Uwazi na Uwajibikaji katika Serikali.
Amesema
kuwa binafsi alikuwa ameamua kukutana na viongozi wa asasi zisizokuwa za kimataifa
wakati wa ziara yake ya karibu katika Afrika ambako miongoni mwa nchi nyingine
alitembelea Tanzania.
Rais
Obama alifurahi sana kukutana na Rais Kikwete. Rais Obama alimkumbatia Rais
Kikwete akimwelezea kama “kaka wa karibu na rafiki mzuri”
kauli na kitendo ambacho kiliwashangaza mamia ya watu waliokuwa kwenye ukumbi.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
23
Septemba, 2013
No comments:
Post a Comment