30 September 2013

MISS KISWAHILI "REHEMA FABIANI" AKIRI KUKAMATWA NA KUWEKWA MAHABUSU KWA WIKI MBILI NCHINI CHINA KWA MADAWA YA KULEVYA

Rehema Fabian.
WAKATI msanii Agness Gerald ‘Masogange’ akisubiriwa kutua Dar baada kumaliza msala wake huko Afrika Kusini, skendo ya baadhi ya wasanii Bongo kuhusishwa na usafirishaji wa madawa ya kulevya ‘unga’, lingine limeibuka ambapo Video Queen Rehema Fabian amekiri kukamatwa nchini China kwa ishu hiyo.

Wiki mbili zilizopita kulizagaa habari kutoka kwa marafiki wa karibu wa Rehema ambao walidai kuwa mshiriki huyo wa Miss Kiswahili 2009 alikamatiwa huko Shaghai baada ya kukutwa na mwanaume aliyekuwa na unga.
Baadhi ya Watanzania waishio China walitofautiana ambapo wakati wengine wakidai kuwa alikamatwa na wapo waliosema kukamatwa kwake kulitokana na kupitiliza muda wa kuishi nchini humo tofauti na viza yake inavyoeleza.
Katika kipindi hicho chote, Ijumaa Wikienda limekuwa likimsaka ambapo wikiendi iliyopita lilifanikiwa kuchati naye ili kupata ukweli wa ‘niuz’ hizo.
mwandishi: Mambo vipi Rehema?

 
Rehema: Mambo poa tu. Nani mwenzangu?
mwandishi: Unachati na gazeti la Ijumaa Wikienda. Kuna taarifa zimezagaa Bongo kuwa umekamatwa na unga China. Hizi habari zina ukweli?
Rehema: Ni kweli nilikuwa mahabusu. Mateso ya huko wee acha tu. Nilipata kesi lakini si yangu ila namshukuru Mungu nimetoka salama.
mwandishi: Kesi inahusu nini na kama ilikuwa haikuhusu kwa nini ulikamatwa?
Rehema: Nilikamatwa na mtu (hakutaka kumtaja na ni nani kwake) alikuwa na unga, nimekaa mahabusu wiki mbili na siku mbili. Uzuri huyo mtu alikataa mbele ya polisi kuwa hanifahamu na sihusiki ndipo nikaachiwa.

-GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname