Ukurasa wa mbele wa gazeti la Risasi la
leo Jumamosi (Sept 14) umetawaliwa na habari inayomhusu msanii wa Bongo
Movie Irene Uwoya yenye kichwa cha habari “UWOYA MBARONI KWA WIZI WA
SIMU!!”.
“MSANII aliyewahi kutamba kisha
kuporomoka kwa kasi katika tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa sababu
ya tabia zake chafu, Irene Uwoya, amefikishwa Kituo cha Polisi Msimbazi
kwa wizi wa simu aina ya iPhone 5.
MAMBO yanaendelea kumwendea kombo
mwigizaji huyo huku akiwa ameanza kuporomoka vibaya kwenye sanaa na
kujikuta akiingia matatani kwa tuhuma za aibu.
Uwoya ambaye siku hizi anajitutumua kwa
kuanzisha kipindi kwenye runinga moja ya Bongo baada ya kushindwa kwenye
filamu, alidakwa na askari wa Kituo cha Polisi Msimbazi, Dar baada ya
kusakwa usiku na mchana kwa kutumia kumbukumbu ya jalada la kesi namba
MS/RB/8522/13 WIZI KUTOKA MAUNGONI.”
Katika kujibu tuhuma zilizoripotiwa
na gazeti hilo, Uwoya kupitia akaunti yake ya Instagram leo amepost
picha ya ukurasa wa mbele wa gazeti hilo wenye habari hiyo pamoja na
maneno yafuatayo:
“Minimti wenye matunda
milele siogop kupigwa mawe…shigongo kamua kunichafua coz nakes nae
mahakaman…anadhan ntaiacha never yeye aponde anavyoweza ila mwisho
wasiku sheria iatafata mkondo wake….minayake mengi nayajua ila ngoja
ninyamaze nisimwagiwe tindikali”

No comments:
Post a Comment