HATARAIIII!!! DAKTARI FEKI ANASWA TENA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI...MAJANGA HAYA...FUATILIA MKASA MZIMA HAPA...
Daktari
anayedaiwa kuwa bandia amekamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
akiwa na vitambulisho bandia vya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili
cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) akisomea Shahada ya Pili.
'Daktari'
huyo ambaye amekuwa akitafutwa na uongozi wa chuo kwa zaidi ya mwaka
alikamatwa jana asubuhi akiwa hospitalini hapo karibu na jengo kilimo
kitengo cha meno.
Katika
kitambulisho chake cha kupigia kura anatambulishwa kwa jina la Dismas
John Macha aliyezaliwa mwaka 1979 Kilimanjaro na anaishi maeneo ya
Upanga Magharibi, Dar es Salaam.
Dismas John Macha baada ya kukamatwa jana.
Paparazi wetu,
alimshuhudia mtuhumiwa huyo akiwa katika kituo cha usalama cha Muhas
na kupekuliwa na askari Polisi Anthony Mwamatepela na kukutwa akiwa na
vifaa vya udaktari.
Baadhi ya vifaa alivyokutwa navyo ni pamoja na
koti jeupe la udaktari na stetoskopu ambacho ni kifaa cha kusikilizia
mapafu yanavyofanya kazi na mapigo ya moyo.
Pia alikuwa na begi jeusi
lenye aina mbalimbali za dawa, vitambulisho na karatasi nyingi, lakini
alipoulizwa alidai kuwa hizo ni dawa zake.
Macha alikutwa pia na
vitambulisho vitatu tofauti, kimoja kikimtambulisha kuwa mwanafunzi wa
Muhas wa Shahada ya Pili ya Udaktari (Masters of Medicine) yenye jina la
Macha Dismas kikionesha kusajiliwa kwa namba 60520/2011 na kumaliza
muda wake Septemba 30 mwakani.
Kitambulisho kingine kilimtambulisha
kwa jina la Macha Rogers anayesoma Shahada hiyo hiyo ikionesha kuwa
anamaliza masomo yake mwakani.
Alikutwa pia na kitambulisho
kinachomwonesha kuwa mwanafunzi wa Shahada ya Kwanza na kadi ya anuani
yenye jina la Amos Nnko ambaye ni Ofisa Rasilimaliwatu wa Chuo hicho.
Akizungumzia
alivyomkamata askari wa chuo hicho, Fulgence Semfukwe alisema
walimkamata baada ya kupata taarifa za yeye kuwa maeneo hayo na kupanga
mbinu za kumkamata.
Alisema saa 4.45 asubuhi jana alimkuta kwenye
jengo la meno na kumwomba kwa nafasi yake ya udaktari amsaidie tatizo
lake na hivyo waongee pembeni, naye bila wasiwasi akakubali.
Alimwuliza anatibu magonjwa gani naye kumjibu anatibu maradhi ya aina nyingi na kumwomba kitambulisho na yeye kumpa cha kwake.
Baada
ya hapo alishituka na kudai kuwa ni daktari wa Mwananyamala na amekuja
hapo kwa ajili ya kuona wagonjwa wake wa dharura ndipo alipokamatwa na
kupelekwa kituo cha Polisi.
Alisema amekuwa akiwachanga kwa muda
mrefu kutokana na kuwa kila walipopewa taarifa yuko wodi au sehemu
fulani hawakumkuta kwani walipishana naye baada ya kuvua koti na kuweka
kwenye begi lake jeusi.
Akizungumza na gazeti hili, Macha limweleza
mwandishi wa habari hizi kuwa yeye ni mwanafunzi ambaye anaelewa masuala
yote ya matibabu, lakini alifeli chuoni hapo mwaka jana.
Alidai kuwa
dawa alizokutwa nazo ni zake kwani ana matatizo katika njia ya mkojo na
kifua huku akiamua kufanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.
"Uwezo wa kutibu ninao na nimesoma katika chuo hiki, lakini mwaka jana nilifeli ndiyo maana nikaamua kuwa hivi," alisema.
Ofisa
Uhusiano wa Muhas, Hellen Mtui alisema kutokana na kukamatwa na nyaraka
akijitambulisha kuwa mwanafunzi wa 'Masters of Medicine', ambaye
anaweza kutibu watu hawana uhakika na idadi ya watu ambao ameshatapeli
hospitalini hapo.
Kuhusu kusoma Muhimbili, Mtui alikana akisema baada
ya kupekua nyaraka za chuo hawakubaini jina la mwanafunzi wa aina hiyo
na katika vyeti vyake bandia vinaonesha kusainiwa na Mkuu wa Chuo
aliyekuwapo kabla chuo hakijapanda hadhi na kuwa chuo kikuu.
Mtui
alisema baada ya kumkamata na kumpiga picha akiwa na mavazi ya udaktari,
kumpekua na kumhoji walimpeleka katika kituo cha Polisi cha Selander
Bridge kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment