Jumatatu ijayo ni siku maalum sana kwa bondia Francis Cheka aliyeitoa
kimasomaso Tanzania hivi karibuni baada ya kumtwanga kwa pointi
Mmarekani Phill Williams 'The Drill' na kutwaa ubingwa wa WBF uzito wa
kati. Cheka, ataanza rasmi pre-form one katika shule ya St. Joseph huko
Morogoro, akisomea masomo ya Kiingereza na Biashara.
Akizungumzia hilo, Cheka amesema "Sikupata elimu nzuri nikiwa mdogo
kutokana na matatizo ya kifamilia, lakini sasa nitaitumia nafasi hii
kujiendeleza zaidi. Nahitaji kuwa Cheka mpya kielimu ili nifike mbali
zaidi, hadi namaliza miaka 10 kwenye masomo yangu nitakuwa na miaka 41
hivyo naweza kuamua kama niendelee na ngumi au nifanye kazi nyingine"
Cheka alijiunga kwenye ngumi za kulipwa mwaka 2000 akitokjea kwenye
ngumi za ridhaa na kufanikiwa kutwaa mikanda ya WBC, IBF afrika, UBO,
IBU, WBO, WBF na ubingwa wa Taifa.
Nini maoni yako kuhusu uamuzi wa Cheka?
source- allanluckyblog

No comments:
Post a Comment