Msanii nyota kwenye tasinia ya muziki na
filamu bongo Zuwena Mohamed “ Shilole” mwishoni mwa wiki iliyopita
alionja joto ya jiwe baada ya kutiwa mtu kati na wakina dada waliokuwa
wanamdai kiasi kikubwa cha pesa.
Habari za uhakika zilizothibitishwa na
mmoja wa wakina dada hao waliokuwa wanamdai zilisema kuwa wanawake hao
waliamua kuchukua hatua za kumtia adabu Shilole baada ya kupata taarifa
kuwa siku hiyo alikuwa ana hama kwa kukimbia na teni lao “ Ishu ilikuwa
hivi sisi tunamdai huyu dada lakini cha kushangaza amekuwa akitupiga
chenga sana na ona alivyokuwa sio mstaarabu kumbe siku hiyo alikuwa
anahama na deni letu ndio maana tuliamua kwenda kumzingua” Alisema dada
huyo aliomba jina lake lihifadhiwe.
Dada huyo aliendelea kufunguka mengi
kuhusu sakata hilo “ Unajua sisi tunafanya biashara zetu hivyo kuna siku
Shillole alikuja na kusema amekwama kipesa hivyo tumuazime pesa na
tukafanya hivyo lakini cha kushangaza mwezi wa sita huu hataki kurudisha
na amekuwa akitukwepa mara kwa mara hivyo majirani ndio wakatushtua
kuwa anataka kuhama kwa staili ya kutoroka na deni letu ndipo tulipoenda
wanawake wanne na kumshushia kipigo” Alisema dada huyo
Baada ya taarifa hizo Shilole alitafutwa
kupita simu yake ya mkononi pamoja na kupita kwenye makoloni yake
hakuweza kupatikani isipokuwa majirani mbalimbali walikili kutokea kwa
tukio hilo la kufedhehesha kwa msanii huyo.

No comments:
Post a Comment