UIMBAJI stadi wa Wibo wa YAHAYA wa Nguli
wa muziki wa Kizaki kipya Lady Jay Dee umemjaza mahela Msanii wa Filamu
aliyejizolea umaarufu kwa miaka ya hivi karibuni, Elizabeth Michael
‘Lulu’ wakati akiimba wimbo huo na Jide wakati wa uzinduzi wa Video yake
mpya na yakwanza kusimama peke yake ya FOOLISH AGE.
Baada ya move hiyo kali ya dakika 120
iliyooesha ukali wa staa huyo kuoneshwa kwa dakika 20 tu na kubakisha
zingine 100 kusubiri wateja kuziona majumbani kwao alipanda jukwaani
kujitambulisha na kutoa shukrani kwa wamepenzi wa tasnia ya filamu
nchini Tanzania kwa muitikio wao alipanda na kuimba wimbo huo wa Yahaya.
Akianzia kuimba kiitikio cha wimbo huo
akiwa Back Stage, Lulu aliwashangaza watu pale alipomudu vyema wimbo huo
kiasi cha mashabiki ‘Mapedeshee’ wakiongozwa na Pedeshee Rich Rich,
kupanda jukwaani na kumtunza fedha kibao ambazo hakika zilimpagawisha
msanii huyo na mwisho wa wimbo huo alisema mziki unalipa.
“Jamanieee kumbe mziki unalipa ile mbaya
yaani nimeimba ubeti mmoja tu hapa ona hela kibao, kuanzia sasa na
mimi nitaanza kuimba mziki”, alisikika Lulu akisenma huku akishangiliwa
na mashabiki wake.
No comments:
Post a Comment