JESHI
la Polisi limeingia katika kashfa nzito baada ya mkuu wake, Inspekta
Jenerali Said Mwema, kuibiwa upanga wa dhahabu ambao ni mali ya
Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za Kusini mwa Afrika
(SARPCCO).
Upanga
huo wenye uzito wa takriban kilo tatu na wenye thamani ya zaidi ya
fedha za Tanzania Sh600 milioni, ni kielelezo kwa nchi inayokabidhiwa
uongozi wa SARPCCO.
Mwaka jana Tanzania ilikuwa mwenyekiti wa SARPCCO, ambapo upanga huo ulikabidhiwa kw
a
IGP Mwema na Jenerali Magwashi Victoria ‘Riah’ Phiyega, ambaye ni
Kamishna wa Taifa wa Polisi wa Afrika Kusini aliyekuwa amemaliza muda
wake kwa wakati huo.
Hilo
ni tukio la pili la wizi la mali zinazohusu ofisi ya IGP, ambapo mwaka
jana ndani ya ofisi hiyo kuliibwa kompyuta ndogo (laptop), ikiwa na
taarifa muhimu za kipolisi. Hadi sasa hakuna taarifa za kupatikana kwa
kompyuta hiyo.
IGP
Mwema alikabidhiwa upanga huo Septemba 5, 2012, katika mkutano saba wa
SARPCCO uliofanyika Zanzibar na kuhudhuriwa na wakuu wa majeshi ya
Polisi kutoka nchi 13, pamoja na mashirika ya kimataifa.
Upanga
huo ambao unakwenda sambamba na bendera ya SARPCCO, ni moja ya
vielelezo vya nchi iliyochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa shirikisho hilo,
ambaye moja kwa moja anakuwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi katika nchi
husika.
Kwa
mujibu wa taratibu za SARPCCO, vielelezo hivyo hutakiwa kuwekwa ofisini
kwa kiongozi husika, ikiwa ni alama ya kila mgeni atakayeingia ofisini
hapo kutambua uwepo wa wadhifa huo wa kimataifa.
Uchunguzi
wa gazeti hili ulibaini kuwa IGP aligundua kutoweka kwa upanga huo wiki
iliyopita, wakati akijiandaa kwenda kuukabidhi kwa mwenyekiti mpya wa
SARPCCO, ambaye ni IGP wa Namibia.
Taarifa
za ndani ya jeshi hilo zilibaini kuwa, IGP alilazimika kuondoka bila
upanga huo alipokwenda Namibia wiki iliyopita kuhudhuria mkutano wa nane
wa SARPCCO, uliofanyika Jumapili iliyopita mjini Windhoek.
Kwa
mujibu wa uchunguzi, IGP Mwema alikabidhi upanga unaofanana na huo
ambao siyo wa dhahabu, alioazimwa kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la
Namibia, Inspekta Jenerali, Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga, na
kukabidhiwa kama ishara ya kukabidhiwa uenyekiti wa SARPCCO kwa kipindi
cha mwaka mmoja.
Uchunguzi
ulibaini kuwa IGP Mwema alitoa ahadi ya kurejesha upanga halisi ndani
ya kipindi cha mwezi mmoja, au Serikali ya Tanzania italazimika
kutengeneza mwingine kulipa uliopotea.
Uchunguzi
wa gazeti hili unaonyesha kuwa kashfa hiyo ametupiwa Mkuu wa Polisi
Zanzibar, Kamishna Mussa Ali Mussa pamoja na dereva wake, ikidaiwa kuwa
upanga huo baada ya kupokewa na IGP Mwema, Septemba mwaka jana uliwekwa
kwenye gari la kamishna huyo. MWANANCHI
its funny kwa kwel., kama na nyie mnaibiwa, how can u protect us!?
ReplyDelete