27 July 2013

MASAI NYOTAMBOFU AFUNGUKA KUHUSU KITU AMBACHO HATASAHAU, NI ALIVYOTOSWA NA DEMU WAKE KISA HANA PESA. SOMA HAPA

Katika interview na mwigizaji wa bongo movies kwa upande wa vichekesho  Gilliady Severine maarufu kama Masai Nyota Mbofu wa Vituko show kwa njia ya simu tokea mkoani Tanga alipo sasa hivi ili tuweze kupata mawili matatu yanayoendelea naye kwa kipindi hiki anachosubiri kufanya video ya wimbo wake mpya na Richie mavoko hivi karibuni. Katika interview hii tulimuuliza mambo mengi sana ila moja ya swali ambalo tulitaka kujua ni jambo gani ambalo hawezi kulisahau tangu alipoingia kwenye sanaa ya uigizaji na muziki.

Masai Nyota Mbofu alisema kuwa katika maisha yake anakumbuka sana tukio la kuachwa kwa kejeli na dharau na mpenzi wake aliyezaa naye mtoto mmoja kisa hakuwa na kitu (Hela) Masai alieleza jinsi ambavyo mrembo huyo aliyemtaja kwa jina moja la Happy la alivyooumiza moyo wake kwa kumdanganya kuwa mtoto (PICHANI) wake huyo aliyezaa naye amefariki dunia ili Masai asiendelee kumsumbua na mpenzi wake huyo mpya. Akiongea kwa huzuni masai amesema akikumbuka huwa anaumia sana kwani alitoka mbali sana a binti huyo na haelewi kwanini aliamua kumfanyia hivyo kisa kapata mpenzi mpya badala ya kumwambia ukweli tuu kwani alikaa kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja akijua motto wake kafariki kabla ya kuja kugundua kuwa yupo hai na mzima wa afya. Masai kwa sasa yupo kwenye maandalizi ya mwisho ya video yake mpya ya muziki unaoitwa "Yero Masai" aliyofanya na Richie Mavoko na kitokolo video itayofanywa na Apex Videos chini ya director Pablo. CHANZO : BONGOMOVIES.COM


No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname