Jina lake anaitwa Danny David ni Mwanamitindo wa kume toka Tanzania na
mwanamitindo pekee toka Tanzania alipata nafasi ya kufanya kazi ya
kutangaza nguo na viatu vya kampuni kubwa ya Adidas tawi la Afrika ya
kusini.
Alianza kuonekana kwenye fashion mwaka 2012 kwenye maonesho ya Swahili
Fashion Week chini ya mwanamitindo maarufu nchini Mustapha Hasanali,
ameshiriki kuonesha mavazi kwenye Harusi fashion week iliyofanyika chini
ya mbunifu wa mavazi Ally Rehmutula na pia alishawahi kushiriki na
kushinda kwenye mashindano ya wanamitindo ya Maridadi model search
yaliyofanyika hapa Tanzania.
Danny ni mwanasheria kitaaluma na ana degree ya sharia toka chuo cha Tumaini Iringa
Katika interview tuliyofanya naye hivi karibuni Danny amesema pamoja na
kuwa mwanamitindo anamipango ya kuwa muigizaji kwani ni kitu alichokuwa
anapenda kukifanya tangu utotoni.
No comments:
Post a Comment