14 June 2013

SOMA HABARI KUHUSU MASELE CHA POMBE.

Habari za uhakika ni kuwa muigizaji wa vichekesho nchini maarufu kwa jina la Masele cha Pombe ni mzima wa afya na hajafariki kama baadhi ya tetesi zilivyoanza kuenea kwa kasi. Swahiliworldplanet baada ya kusikia tetesi kuwa Masele amefariki kwa ajali ya gari jioni hii huko Tanga ilibidi kutafuta ukweli kuhusu muigizaji huyo maarufu na kufanikiwa kupata habari za kina kupitia Kabuti Onyango ambaye ni cameraman maarufu wa filamu za kitanzania. Kabuti ambaye ni mtoto wa Mzee Onyango ambaye ni muigizaji mkongwe http://audifacejackson.blogspot.com/

nchini amesema kuwa amezungumza na baba yake(Mzee Onyango) muda mfupi uliopita ambaye yupo Tanga na jibu ni hili " baba yupo Tanga mzee onyango na nime mpigia simu kaniambia kwamba walikuwa na masele kwenye hilo gari lakini si kwamba amefariki hapana ila masele aligonga mtu akakamatwa na raia wakavunja kioo na kutaka kumuua aligonga mtu wa kwanza na akataka kukimbia akagonga mwingine ndio ilivyo kuwa lakini ni mzima na yupo kituo cha police"




Alisema kuwa kama ni kuumia basi atakuwa amepata majeraha madogo tu.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname