MTANGAZAJI maarufu wa Clouds FM,
Gerald Hando leo alfajiri alizua kizaazaa na kupelekea kutishiwa bastola
na mtu ambaye jina lake halikufahamika mara moja.
Chanzo kimesema Hando aligonga gari
la mtu huyo maeneo ya Kwa Kopa, jambo lililopelekea mtu huyo ashuke
kwenye gari lake bastola ikiwa mkononi na kutishia kumfumua Hando.
Kama mtu huyo alidhani kutoa bastola
ndio suluhisho basi alikosea sana, Gerald Hando anayetangaza kipindi cha
"Power Breakfast" naye alishuka kwenye gari lake na kufungua shati lake
na kuanza kumuamrisha mtu huyo afyatue bastola.
Huku akiporomosha matusi kwa ukali Hando alisema: “Piga hiyo bastola yako, shoot me.”
Hando aliendelea kuwa mkali huku
akipigapiga kifua chake hali iliyovuta watu wengi kwenye tukio hilo
ambao waliwasihi wote wawili kutuliza mzuka na kumfanya mtu huyo
aliyekuwa na gari aina ya Rav 4 arudishe bastola yake kwenye gari na
kutafuta njia nyingine ya kulimaliza tatizo lililotokea.
No comments:
Post a Comment