14 June 2013

ANGALIA PICHA JINSI KALA JEREMIAH ALIVYOMKABIDHI TUZO MAMA WA MANGWEA,NA ALIPOTEMBELEA KABURI LA MAREHEHU NGWEA

Mama mzazi wa marehemu Albert Mangweha akiwa ameshikilia tuzo aliyopewa kwa niaba ya mwanae, tuzo hii aliipata msanii Kala Jeremiah kwenye tuzo za Kilimanjaro ikiwa kama tuzo ya msanii bora ya Hip Hop 2013-14




1 comment:

  1. MKAKATI MZITO WA KUMMALIZA LADY JAYDEE BADO UNAENDELEA…

    PAMOJA na kumshtaki mahakamani kuwa amewakashifu, sijaelewa kwanini Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga bado wanamuandama Lady Jaydee. Ingawa hawako wazi, lakini kiukweli wako nyuma ya shoo zote zilizoibuka ghafla baada ya Jaydee kutangaza shoo yake ya kuadhmisha miaka 13 tangu alipoanza muziki. Lengo nadhani ni kuhujumu shoo yake.
    Hilo si neno sana kwa kuwa nao bado wanahangaika kutafuta hela.
    Kinachonishangaza ni hiki kinachoendelea kwa sasa. Nimeamua kukizungumza baada ya shoo zote kuwa zimeshakamilika maandalizi yake, sijali nani atapata watu wengi kwenye shoo yake na nani ataathirika kwani wote wanatafuta.
    Nipo karibu sana na hawa kina Ruge, wamefanya wanayoyafanya, mengine yanayolalamikiwa yakiwa ya kweli, mengine yakiwa yanaongezwa chumvi mno kwani nipo karibu nao sana. Ila mengi ni ya kweli ya chumvi ni kidogo sana.
    Baada ya ugomnvi wao na Jide kuripotiwa sana, huku baadhi ya vyombo vya habari vikiwatupia lawama, hawa jamaa sasa wanadhani baadhi ya vyombo vya habari vimelipwa na mmoja wa wamiliki wakubwa wa vyombo vya habari nchini ili kutumia ugomvi wao na Jide kuwamaliza ‘eti’ kwa kuwa redio yao ina nguvu. Hili linachekesha kidogo kwa vile ninavyojua redio yao haitii mkono kabisa kwa huyo wanayemtuhumu.
    Naamini hilo.
    Pia, wanadai mmiliki huyo yuko nyuma ya magazeti yanayoripoti ishu ya vita yao na Jide. Wanadai vita ya redio kwao haiwatishi, hivyo wameamua kumalizana na magazeti ili yasiendelee kuandika kabisa lolote kuhusu Lady Jaydee.
    Tayari wameshawaita baadhi ya wahariri wa magazeti hasa ya udaku na kumalizana nao. Kama hamuamini, fuatilieni magazeti haya yaliyokuwa yakiripoti sana habari hizo, kama yataamuandika tena Jaydee labda kwa mabaya. Hata shoo yake inaweza isifanyiwe coverage kabisa.
    Ninazo picha nilizowapiga hawa jamaa wakiwa na mkutano na wahariri wa magazeti haya. Namuomba Lady Jaydee amuone waziri wa habari vijana na utamaduni kuingilia sakata hili kwani anao uhuru wa kuandikwa habari zake kama msanii. Nitakuwa tayari kuwasilisha ushahidi wa picha nilizowapiga na tape niliyorekodi mazungumzo waliyoyangea wakiwa na wahariri hawa kwenye mpango wao mchafu. Kikao kilifanyika Sinza kikiratibiwa na mtu aitwaye Abdallah Mrisho.
    Huu ni uhuni uliopitiliza.
    Hawa jamaa ni watu wangu wa karibu, niliamua kujitoa mhanga kuwapiga picha na kuwarekodi kwa maslahi ya vijana wengine wanaobaniwa, na si kwa ajili ya Lady Jaydee pekee.
    Lady Jaydee hivi uliwalia nini chao kikubwa hawa jamaa mpaka wakuandame namna hii?
    Nitaendelea kushusha data za kila wanayoyafanya.
    NIMEAMUA!!!!
    Stay tuned Q Chillah. Jipange na hawa jamaa!

    ReplyDelete

Comments system

Disqus Shortname