25 May 2013
Yule Kijana Rama mla Watu Aliyekamatwa na Kichwa cha Mtu Aachiwa Huru-Soma Story Hapa
Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imeamua kumuachia huru Ramadhani
Selemani Mussa ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya kukutwa na kichwa
cha mtu. Rama, ambaye muda wote huo alikuwa rumande gereza la Segerea
akisota kusubiri hukumu yake, alikamatwa hospitali ya Muhimbili mwaka
2008 ambapo pia alikiri kuwa alikuwa na tabia ya kula nyama za watu
ambayo amefundishwa kichawi toka alipokuwa mdogo. Mahakama imemuachia
huru kwasababu mtuhumiwa alitenda kosa hilo pasipo kuwa na akili timamu.
Hata hivyo mahakama hiyo imetoa agizo la kuendelea kumuweka kijana huyo
katika hospitali ya wagonjwa wenye matatizo ya akili, hospitali ya
Isanga iliyopo Dodoma mpaka pale atakapona ndipo aruhusiwe kurudi
mtaaani.habari kutoka karibu ndani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment