Msanii
wa muziki wa kizazi kipya ajulikanae kwa jina la Snura akiimba jukwaani
wimbo wake unaotamba kwa sasa katika vituo vingi vya redio,uitwao
Majanga,mbele ya maelfu ya watu waliofika kwenye uwanja wa Jamuhuri
jioni ya jana wakati wa kituo cha redio ya Clouds FM ilipokuwa ikizindua
msimu wake mpya kwa wasikilizaji wake, uzinduzi huo ulikwenda sambamba
na kufanyika kwa semina ya fursa kwa Watanzania.
Aidha msimu huo umekwenda
sambamba na kaulimbiu inayofuatia harakati za MADE IN TANZANIA, ambapo
msukumo wake ni kuwashawishi Watanzania kuanza kuzifanyia kazi fursa
hizo kwa umoja wa maendeleo ,huku neno TWENZETU likitumika kama neno
rasmi la mawasiliano.Kama vile haitoshi uzinduzi huo utabeba harakati
rasmi za vita dhidi ya Uharamia wa kazi za wasanii,Wabunifu na wavumbuzi
mbalimbali.
Leo Jumapili kutakuwepo na
matembezi ya kampeni ya kupinga uharamia wa kazi za sanii yatakayoanzia
uwanja wa Jamuhuri mapema asubuhi na kupokelewa na Waziri Mkuu Mh.
Pinda.
Msanii mahiri wa Mashairi
hapa nchini, Mrisho Mpoto akiwakuna vilivyo wakazi wa mji wa Dodoma jana
jioni alipowaangushia maneno kadhaa na umati kulipukwa na mayowe kila
kona, ambapo Clouds FM wamezindua msimu wao mpya.
Maelfu ya Watu wakiwa ndani
ya uwanja wa Jamuhuri jana jioni wakijumuika kwa pamoja na wana Clouds
FM walipokuwa wakizindua msimu wao mpya.
Msanii wa muziki wa kizazi
kipya a.k.a bongofleva katika miondoko ya Hip Hop, Izzo Bizziness
akikamua kwa shangwe kubwa mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Dodoma
waliofika ndani ya uwanja wa Jamuhuri, walipokwenda kushuhudia uzinduzi
wa msimu mpya wa Clouds FM.
Msanii wa muziki wa kizazi
kipya,Madee akitumbuiza mbele ya umati mkubwa wa watu ndani ya uwanja wa
Jamuhuri,wakati wa kituo cha redio ya Clouds FM kilipokuwa kikizindua
msimu wake mpya.
Pichani shoto ni Mkurugenzi
wa vipindi na Utafiti, Ruge Mutahaba akizungumza na Katibu wa
NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye ndani ya Uwanja wa Jamuhuri Jana jioni
wakati tamasha la uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM likiendelea, Nape
alifika uwanjani hapo kujionea shamrashamra mbalimbali zilizojumuisha
maelfu ya watu.
Palikuwa hapatoshi uwanja wa jamuhuri Dodoma jioni ya leo.
Msanii
wa mkongwe wa muziki wa kizazi kipya a.k.a bongofleva katika miondoko
ya Hip Hop,Afande Sele a.k.a Baba Tunda akikamua kwa shangwe kubwa
mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Dodoma waliofika ndani ya uwanja wa
Jamuhuri,walipokwenda kushuhudia uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM.
No comments:
Post a Comment