Mwanaharakati
maarufu wa haki za mashoga nchini Zambia Paul Kasonkomona amekamatwa na
polisi baada ya kuonekana akifanya mahojiano katika kipindi cha ‘Live’
katika luninga
moja nchini humo akihamasisha mahusiano ya jinsia moja
yahalalishwe.
Mkuu
wa polisi Solomon Jere amekaririwa akisema Paul Kasonkomona
ameshitakiwa kwa kuihamasisha jamii kushiriki katika katika matendo
yasiyokubalika.
Alitiwa kizuizini wakati akitoka katika studio za televisheni hiyo inayomilikiwa na Muvi TV katika jiji hilo.
Vitendo vya mahusiano ya jinsia moja nchini humo ni kinyume cha sheria za Zambia.
Hata hivyo baadhi ya wananchi nchini humo wanachukulia hatua hiyo kama kinyume na haki zao.
No comments:
Post a Comment