Mwanamuziki
toka mkoani Morogoro anayefanya poa kwa sasa na wimbo wake
wa Leo mwanadada Dayna Nyange a.k.a Mkali wao, amefunguka na
kumpigia saluti mwanamuziki mkongwe toka hapa Morogoro Afande Sele.
Akiongea na mwandishi wetu
toka jijini Mwanza aliko sasa katika ziara ya kimuziki na
uzinduzi wa Albam ya Kala. Dayna amesema huwa anamkubali afande
kwa tungo zake
''
kwa kweli siku zote, nimekuwa nikimkubali sana Afande sele
kwa tungo zake zenye ujumbe, lakini kwa wimbo huu wa Dini
tumeletewa, nampigia saluti.
Afande ni bonge la msanii na huwa
naskiliza nyimbo zake kwani najuwa nikiskiliza nyimbo zake kuna
madini napata, lakini sasa kaka mkubwa kwa hapa alipofikia na
kufikilia kwa kina juu ya wimbo huu, anastahili kuwa mfalme wa
Rhyme, waliompa tuzo hawakukosea.
Big
up sana Afande, saluti kwake, aendelee kuwa mwalimu wa ujumbe ,
huuwimbo ni zaidi ya Hotuba ya kitaifa Inayotolewa na Rais''
Amesema Dayna
Ubalozini
No comments:
Post a Comment