Jeneza la aliyekufa kwa ugonjwa tayari limetolewa pembeni. Sasa anafukuliwa aliyezikwa akiwa hai
Mwili wa aliyezikwa hai unatolewa kaburini
Dada wa marehemu aliyezikwa akiwa hai
Mwili
wa marehemu aliyezikwa hai baada ya kutolewa kutoka kaburini. Pembeni
ni jeneza la marehemu aliyetuhumiwa kumuua kwa ushirikina
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kijiji na kata ya
Mkwajuni Wilaya ya Chunya Mkoani hapa wamemzika Mwanakijiji mwenzao
akiwa hai wakimtuhumu kusababisha kifo cha Mkazi mmoja kijijini hapo.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Apri 26 mwaka huu majira ya Saa
Nane Mchana katika Kitongoji cha Maweni Makaburini baada ya Mhanga
aliyefahamika kwa jina la Victory Mwachirui(68) kuhudhuria mazishi ya
Pita Barton(28)aliyefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Thobias Ismail amesema
marehemu alipatwa na umauti akiwa anapatiwa matibabu kwa mganga wa jadi
ambaye jina lake halikuweza kujulikana maramoja.
Amesema wakati taratibu za mazishi zikiendelea Ndugu wa marehemu
walidai kuwa kifo cha Marehemu kilisababishwa na Mwachirui ambaye ni
Katekista mstaafu kwa imani za kishirikina.
Ameongeza kuwa wakati kaburi likichimbwa kwa ajili ya kumzika
marehemu ndipo vijana waliokuwa wakichimba waliagiza Wazee wa Mila
wafike makaburini kwa ajili ya kuangalia utaratibu wa mazishi na kukagua
ukubwa wa Kaburi ambalo lilikuwa limekwisha chimbwa.
Kutokana na mwito huo walifika wazee wanne akiwemo Mzee Mwachirui
ambaye walimsisitiza kusogea jirani na kaburi ambapo baada ya kusogea
alipigwa na Sururu kichwani na kuangukia kaburini huku akisindikizwa na
marungu.. Kwa habari kamili na picha zaidi, click link ifuatayo
source-laivu.com
No comments:
Post a Comment