MAZISHI ya msanii mahiri wa tasnia ya filamu Juma Issa Kilowoko
‘Sajuki’ anatarajia kuzikwa siku ya Ijumaa mchana katika makaburi ya
Kisutu baada ya sala ya Ijumaa, akiongea na FC leo Rais wa shirikisho la
Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba amesema kuwa msiba huu unasimamiwa na
shirikisho na wasanii wa filamu na wadau wa tasnia ya filamu.
“Tumeamua kulichukua jukumu la kumzika msanii mwenzetu Sajuki na
familia wabaki na shughuli nyingine kwa sababu amemwacha mke na motto
ambao kwa vyovyote watahitaji kuishi kwa hiyo kama kuna kidogo basi
kiwasaidie, kwa hiyo tayari kuna kamati inayoshughulikia hilo,”anasema
Mwakifwamba.
Rais wa TAFF alimedai kuwa bajeti ya awali kuanzia leo hadi siku ya
mazishi gharama au fedha inayohitajika ni milioni Saba ambazo wadau
mbalimbali na wasanii bado michango inahitajika hivyo Mwakifwamba
anaomba wale wote wanaoguswa na msanii huyo hata kama si wasanii lakini
wana michango yao wafike msibani na kuwakilisha michango hiyo.