26 January 2013

Risasi na mabomu vinarindima hivi sasa Tandika

Habari ambazo zinaingia hivi sasa toka kwa mwanahabari Iddy Mkwama, zinaeleza kuwa
Risasi na mabomu yanarindima Tandika kutawanya wananchi wenye hasira,,inasemekana ni baada ya mtu mmoja anayejulikana kwa jina la
Mang’ana (mkurya) kumpiga risasi jirani yake,, wananchi wakaamua kufanya vurugu kwenye nyumba ya aliyefanya tukio,,askari wa FFU wapo eneo la tukio…habari za awali zinadai mtu huyo kapigwa risasi baada ya kukataa kulipia huduma ya maji ambayo ndoo moja haizidi shilingi 50.
Endelea kuwa nasi kupata updates
UPDATES: Shuhuda mmoja wa tukio hili aliyeko eneo la tukio ametutumia ujumbe ufuatao:
“Kaka, kuna vurugu sana. Nimeondoka eneo la tukio, ila huyo aliyepiga mtu risasi anauza maji nyumbani kwake. Inasemekana baada ya kurudi nyumbani kake, mkewe akamwambia kuna kijana wa jirani amechota maji hajalipa, anadaiwa shilingi 100. Yule bwana akatoka na bastola akampiga risasi ya mbili (kijana anayedaiwa hela ya maji), zikamkosa na ya tatu ikampiga mguuni.
Askari waliondoka eneo la tukio kwenda kumpeleka mtuhumiwa kituoni huku nyuma, vibaka wakaanza kuvunja mageti. Wameiba vitu vya ndani na punde zimerejea gari mbili za polisi mabomu yameanza tena. Mitaani vijana wanapita wakiwa na vitu walivyochukua kwenye nyumba ya huyo jamaa na kwa hasira wanazozionyesha, kuna uwezekano nyumba yenyewe ikachomwa moto maana tayari gari lake aina ya Nissan limevunjwa vioo”
source-jukwaahuru

Comments system

Disqus Shortname