08 January 2013

HUYU ndo MSANII WA BONGO FLAVOUR ALIYE FARIKI DUNIA ..SIKILIZA WIMBO WAKE -ANAITWA OMARY OMARY - MAJALIWA

MSANII  nyota wa miondoko ya Mnanda a.k.a Mchiriku, Omari Omar amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Habari zilizoifikia , asubuhii zinasema kuwa, Omar Omar aliyetamba na nyimbo mbalimbali ukiwemo ule maarufu wa 'Kupata ni Majaliwa' alifariki nyumbani kwao Temeke, saa chache baada ya kurejeshwa toka hospitali ya temeke alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.
Taarifa hizo zinasema kuwa mara baada ya kurejea nyumbani, msanii huyo alizidiwa na hatimaye kufariki na kwamba msiba wake upo nyumbani kwao Temeke Mikoroshini kwa ajili ya mipango ya mazishi.
Msiba wa msanii huo umekuja siku chache baada ya tasnia ya sanaa na burudani kumpoteza Juma Kilowoko 'Sajuki' msanii nyota wa filamu aliyefariki pia kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya muda mrefu.
TheChoiceTz inawamuombea kila la heri Omar Omar na wengine waliotangulia mbele ya haki mapumziko mema katika safari yao ya Ahera. Innallillah Waina Illah Rajiun.
Taarifa zaidi tutakuwa tunawaletea kujua mkali huyo wa mduara aliyewafanya wasanii wengine kufuata mkondo wake akiwemo Dogo Mfaume, Ferouz, Easy Man na wengin source mcharazo

Comments system

Disqus Shortname