Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mh. Frederick Sumaye.
Baadhi
ya majina makubwa yaliyopoteza uchaguzi ni Waziri Mkuu mstaafu
Frederick Sumaye, Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na
Michezo Amos Makalla na Mbunge wa Jimbo la Igalula Dkt. Athumani Mfutakamba aliyeambulia kura 231 akiangushwa na Mtendaji wa Kata.
Michezo Amos Makalla na Mbunge wa Jimbo la Igalula Dkt. Athumani Mfutakamba aliyeambulia kura 231 akiangushwa na Mtendaji wa Kata.
Katika
chaguzi hizo Mbunge wa zamani wa Jimbo la Nyamagana Lawrence Masha
amepata ushindi wa kishindo na kuukwaa Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa (NEC).
Waziri
wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dk Mary Nagu
ambaye pia ni Mbunge wa Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara ameibuka
kidedea na kumshinda mpinzani wake Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye.
Msimamizi
wa uchaguzi huo Elaston Mbwilo alisema kuwa Dk Nagu aliibuka kidedea
kwa kupata kura 648 ambapo mpinzani wake Frederick Sumaye aliambulia
kura 481 kati ya kura 1129 zilizopigwa ambapo kura 41 ziliharibika.