16 October 2012

Aliyezusha Balozi wa TANZANIA nchini MALAWI kafukuzwa, akamatwa na Polisi.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, kulikuwa na taarifa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Patrick L. Tsere amepewa barua na Serikali ya Malawi inayomtaka kuondoka nchini humo ndani ya saa 48 kutokana na maoni yanayohusiana na mipaka ya Ziwa Nyasa/Malawi aliyoyatoa redioni alipokuwa akizungumza katika mahojiano na kipindi kimoja cha redio ya Zodiac ya nchini humo.

BBC Swahili katika kipindi chake cha Dira kimerusha mahojiano yake na Balozi Tsere kuhusiana na taarifa hiyo.

Balozi amesema aliyetoa chapisho hilo amekamatwa na Polisi wa nchini Malawi, ingawaje huo siyo uthibitisho kuwa kukamatwa kwake kunatokana na chapisho husika lililotoa uvumi ambao umekanushwa pia na Serikali ya Malawi.

Comments system

Disqus Shortname