SIKU
chache baada ya kuahidi kumzalia mtoto mpenzi wake aliyemtaja kwa jina
la Bushoke, mwigizaji wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’
amedaiwa kupata tatizo la mimba yake kuharibika.
Chanzo chetu kimetutonya kuwa, kuharibika kwa mimba hiyo
kulibainika hivi karibuni huku mwenyewe akieleza kutojua sababu.
“Mwenyewe anadai hata hajui imeharibika kwa sababu gani lakini ukweli
ndiyo huo.Hata alipohojiwa na Clouds Tv juzi alishindwa kunena
ukweli.Kwa sasa hana raha kabisa kwani alishaamua kuzaa lakini ndiyo
hivyo tena,” kimedai chanzo hicho.
Katika kupata ukweli wa habari hiyo, mwandishi wetu amemtafuta Jini
Kabula na alipoulizwa juu ya mimba yake kuchoropoka amesema kwa
masikitiko:
“Naomba unipigie baadaye nitakueleza kila kitu lakini ni ukweli kwamba ‘mwanangu’ ametoka.”
No comments:
Post a Comment