13 September 2012

Fid Q afikiria kuwapeleka kortini Orijino Komedi kwa kumchafua


Baada ya Orijino Komedi kumshutumu rapper Fareed Kubanda aka Fid Q kuwa amecopy na kupaste beat ya wimbo wake Danger, rapper huyo hajaridhika na hatua zilizochukuliwa mpaka sasa kiasi cha kufikiria kutafuta mwanasheria ili
awaburuze kortini waigizaji hao.
“Looking for a good lawyer dealing with defamation of character cases.. Contact us for details,” Fid alitweet jana.
Baada ya kuona tweet hiyo, Bongo5 ilimpigia simu rapper huyo kutaka kujua kama kweli amedhamiria kulipeleka suala hilo kwenye sheria na yeye kusema kuna watu walimshauri afanye hivyo lakini ameamua kupuuzia.
source-bongo5

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname