23 July 2012

Mkurugenzi Mtendaji NBC asimamishwa kazi


Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya NBC imemsimamisha kazi kwa kumpa likizo Mkurugenzi Mtendaji wa  benki hiyo , Lawrence Mafuru (pichani)kupisha uchunguzi wa kukiuka taratibu za utendaji ndani ya taasisi hiyo maarufu ya fedha nchini.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa jana na benki hiyo na kutiwa saini na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Mussa Assad,  uamuzi huo ulichukuliwa kufuatia malalamiko ya wafanya wa NBC  yakimtuhumu Mkurugenzi huyo kuwa alikuwa anakiuka taratibu za kiutendaji.
“Bodi ya Wakurugenzi wa NBC imepokea malalamiko ya wafanyakazi kuhusu kuwapo ukiukwaji mkubwa wa taratibu za kiutendaji katika uongozi wa benki.” 
Alisema Assad katika taarifa hiyo na kuongeza:“NBC ni benki inayoheshimika na kuaminika,  kwa hiyo ili ya kulinda taratibu na misingi ya utawala bora, imeanza kufanya uchunguzi wa kina na sahihi juu ya tuhuma hizo.
Ili kufanijkisha kazi hiyo, Bodi ya Wakurugenzi  imeamua kumpa likizo Mafuru ili kupisha uchunguzi huo kufanyika. Naamini kazi hiyo itakamilika mapema iwezekanavyo.”

Naye mafuru kwa up-ande wake alisema; “ Nitatoa ushirikiano kwa dhati kuhakikisha kuwa uchunguzi  juu ya  tuhuma zinazonikabili unafanyika kwa uhuru na haki.”

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname