WAKATI kocha
Mserbia Milovan Cirkovick ameondoka kurejea kwao kwa mapumziko mafupi,
klabu ya Simba inasaka beki wa kati, beki wa kulia, beki wa
kushoto na mshambuliaji mmoja, lakini wote watakuwa wachezaji wazawa,
imeelezwa.
Habari za ndani kutoka Simba SC, zimesema kwamba baada ya
kutolewa katika Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame,
pamoja na kugundua hawakuwa na maandalizi ya kutosha, lakini pia wamebaini
mapungufu kikosini.
mapungufu kikosini.
“Tunahitaji beki wa kulia mmoja, kwa kuwa kipindi hiki beki
wetu mwingine wa kulia Chollo (Nassor Masoud) ni majeruhi, anabaki Kapombe
(Shomary) pekee, tunahitaji beki wa kushoto, kwa sababu Amir Maftah ni majeruhi
pia, anabaki Paul Ngalema pekee. Tayari mchakato umeanza,”kilisema chanzo
kutoka Simba SC.
Aidha, chanzo hicho kimesema Simba pia inasaka beki wa kati
mzalendo, kwa kuwa mabeki wake wa kati iliyonao kwa sasa, Lino Masombo, Juma
Nyosso na Obadia Mungusa wote ni wa aina moja, hivyo wanasaka beki wa aina
tofauti na hao.
Alisema Simba inaendelea pia kusaka mshambuliaji mwingine mzawa
kuongeza nguvu kwenye safu hiyo ambayo hadi sasa inao Felix Mumba Sunzu, Danny
Mrwanda na Abdallah Juma.
“Kama tutamuuza Okwi (Emmanuel) ina maana tutaweza kusajili
mshambuliaji mwingine wa kigeni na kwa kweli mrithi wa Okwi lazima Okwi
mwingine au zaidi ya Okwi, kwa sababu hadi sasda katika mashindano haya
(Kagame) hatujaona mchezaji wa kiwango cha Okwi,”kilisema chanzo hicho.
Okwi, anaendelea na majaribio katika klabu ya FC Red Bull
Salzburg ya Austria na majibu yake yanatarajiwa kutolewa wiki ijayo na iwapo
atafuzu, Simba italipwa Euro 600,000.
Simba ilitolewa juzi katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa ya
soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, baada ya kufungwa na Azam FC
mabao 3-1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mbaya wa Simba juzi alikuwa John Raphael Bocco ‘Adebayor’
aliyefunga mabao yote matatu, wakati bao la kufutia machozi la Simba lilifungwa
na Shomary Kapombe.
Wachezaji wote wa Simba wamepewa likizo ya wiki moja na
kocha Profesa Milovan Cirkovick anarejea kwao Serbia kwa mapumziko mafupi
atarejea wiki ijayo kuendelea na kazi.
Profesa Milovan akirejea ataanza kuandaa timu kwa ajili ya
msimu mpya wa Ligi Kuu, na kikosi kipya cha Simba iliyoboreshwa kitaonekana kwa
mara ya kwanza katika tamasha la kila mwaka la kuazimisha kuzaliwa kwa klabu
hiyo, Simba Day, ambalo na mwaka huu tena litafanyika Agosti 8, Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Wakati huo huo; Habari zaidi kutoka Simba SC zinasema kwamba, iwapo
URA haitamnunua beki Haruna Shamte, basi atatolewa tena kwa mkopo kwa kuwa
hajamvutia kocha Milovan kwa uchezaji wake. Aidha, Victor Costa naye ametemwa rasmi na yuko huru kujiunga na timu nyingine yoyote.
SOURCE -BIN ZUBERY
No comments:
Post a Comment